feedburner
Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

feedburner count

Tanzania: Richard cautions Latoya

Labels: , ,


Richard amuonya Latoya BBA3


na Khadija Kalili


MSHINDI wa shindano la Big Brother II mwaka jana, Richard Bezuidenhout, ametoa ushauri wa bure kwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la mwaka huu BBA 3, Latoya Lyakurya, kuwa mwangalifu na kubadili tabia yake endapo anataka kuendelea kukaa katika jumba hilo.

Akizungumza kwenye kipindi cha ‘Jambo Afrika’, kinachorushwa na Televisheni ya TBC 1, juzi, Richard alisema kwamba mshiriki huyo amezidi kuwa mapepe, hivyo apunguze.

“Jambo jingine analolifanya ni kutudhalilisha Watanzania, hivyo aelewe kwamba ukiwa machachari sana, watu huchoshwa na wewe, hivyo wanaweza kukupigia kura za kukutoa kwenye jumba,” alisema Richard.

Latoya ambaye amepigiwa kura za kutolewa kwenye shindano hilo, pamoja na mshiriki mwingine Tayana hatima yao iko mikononi mwa mashabiki wa nchi wanazotoka, hivyo wameombwa wawapigie kura ili kuwanusuru.

“Katika hali isiyo na kificho, hatima ya Latoya kubaki BBA3 iko mikononi mwa Watanzania, hivyo wamnusuru kwa kumpigia kura kwa njia ya ujumbe mfupi,” alisema Richard.

Jumapili iliyopita, Latoya na Tawana walitolewa kwenye jumba hilo na kuweka kwenye shimo la taka, ambako mmoja kati ya wawili hao atatoka na mwingine kurejea jumbani Jumapili ijayo.

Aidha watazamaji wa shindano la BBA 3, linalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini juzi walianza kupiga kura ya kuchagua mshiriki atakayerudishwa kwenye jumba hilo kutoka katika shimo la taka, ambako wametenganishwa huku wakishuhudia kila kitu kinachoendelea kwenye jumba hilo.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/9/17/habari71.php

English translation:(translation courtesy of Dudumizi)

Richard Cautions Latoya

The winner of last year's Big Brother II, Richard Bezuidenhout, has offered free advice to Tanzania's representative to BBA 3, Latoya Lyakurwa, to be careful and change her behavior if she'd like to stay in the Big Brother House.

Speaking on "Jambo Afrika" programme on TBC1, Richard said Latoya should reduce being silly.

"Another thing she is doing is disgracing Tanzanians, so she should know that if if you become too restless viewers become tired of you and can vote you out", said Richard.

Latoya, who has been nominated for possible eviction, together with Tawana, have their fate in fans from the countries they are coming from, so they have been asked to vote to save them from eviction.

"What is very clear is that Latoya's fate is is the hands of Tanzanians. So they (Tanzanians) must send SMS to rescue her", said Richard.

Last Sunday Latoya and Tawana were removed from Big Brother's house and placed in the rubbish dump where next Sunday one of them will be evicted and the other will go back to Big Brother's house.

§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§§

I AM IMPRESSED! These are the words of a married person who had an open relationship in BBA II... And now he has the nerve to criticise a housemate who, at most, has shared a bed with and kissed two men (Not sure if she had gotten intimate with any!)

Technorati Tags: ,






0 comments:

Post a Comment